Wanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Alikiba na Diamond wanatarajia kupambana kwenye utoaji wa tuzo za AFRIMA zitakazofanyika nchini Nigeria.

Alikiba na Diamond watapambana kwenye kipengele cha Msanii bora wa kiume kutoka Afrika Mashariki ambapo ndiyo wasanii pekee waliofanikiwa kuingia kwenye kipengele hicho.

Majina ya wasanii hao waliochaguliwa kwenye vipengele mbalimbali vya tuzo za AFRIMA 2017 yametangazwa jana usiku.

Wasanii wengine kutoka Tanzania waliotajwa kwenye tuzo hizo ni Lady Jaydee, Nandy na Vanessa Mdee wote wapo kwenye kipengele cha msanii bora wa kike kutoka Afrika Mashariki.

Upigaji kura wa Tuzo hizo utaanza Tarehe 21 Agosti mwaka huu na zitatolewa tarehe 12 mwezi Novemba huko Lagos nchini Nigeria, Tazama Orodha kamili ya tuzo za AFRIMA 2017 hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *