Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuanza kufanya ziara za kukagua maendeleo ya wanafunzi kwa kupita madarasani.

Amewataka viongozi hao kuhoji kama wanafundishwa kulingana na maelekezo ya mitaala badala ya kusubiri ripoti kutoka kwa walimu ambazo wakati mwingine hutoa majibu ya uongo.

Waziri Simbachawene ametoa agizo akiwa kwenye ziara ya kikazi Wilayani Mpwapwa ambapo amesema ni wajibu kwa wakuu hao pamoja na viongozi wa halmashauri kujenga utamaduni wa kuwaona wanafunzi katika maeneo yao na kuhakikisha wanapata elimu sahihi iliyokusudiwa na serikali na jambo hilo halihitaji taaluma ya ualimu kwakuwa viongozi wote wanaosimamia wanajua kusoma na kuandika.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Donard Ng’wenzi amemueleza waziri kuwa halmashauri hiyo imesitisha kupitisha fedha za utekelezaji wa miradi ambayo imetekelezwa chini ya kiwango akitolea mfano mkandarasi ambaye aliyekua anafanya ujenzi wa Zahanati ya Singonali ambaye ametoweka kusiko julikana baada yakupokea kiasi cha mhilingi milioni 48.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *