Viongozi  wa Kamati ya Utendaji ya Yanga wameigomea barua ya kujizulu waliyoandikiwa na mwenyekiti wao, Yusuf Manji na kumuomba abatilishe uamuzi wake huo ili aendelee kuongoza.

Manji, Jumanne iliyopita aliandika barua ya kujiondoa nafasi hiyo huku akitaja sababu kubwa ni kuwapisha watu wengine wapya waiongoze timu hiyo kwa mafanikio.

Wakati anaaga kuondoka, siku hiyohiyo Wenyeviti wa Matawi ya Yanga haraka walikutana kwenye makao makuu ya klabu hiyo kwa ajili ya kupinga uamuzi huo wa Manji.

Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga amesema kuwa walikutana na kufanya kikao cha dharura kujadili uamuzi huo wa mwenyekiti wao.

Mtoa taarifa huyo alisema katika kikao hicho wajumbe hao kwa pamoja walikubaliana kukutana na Manji kumuomba aendelee kuiongoza timu hiyo kwa kipindi chote alichokibakiza.

Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa kuzungumzia hilo amesema kuwa suala hilo la kikao cha dharura kufanyika kwa wajumbe ni kweli walikutana na kwa upande wake alisema hawezi kulizungumzia hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *