Baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu wamemmjia juu mwanamuziki Diamond kutokana na kuimba wimbo ‘Hallelujah’ pamoja na kuvaa cheni za msalama kwenye video zake.

Mmoja wa sheikh hao, Sheikh Kipozeo amesema kuwa Diamond hajafanya vizuri kuimba  wimbo huo  kwa sababu huku ni kama kukiuka imani yake ya dini ya kiislamu na kumsujudia nabii Issa.

Sheikh Kipozeoa amesema kuwa Kitendo cha kuvaaa msalaba kilichoonyeshwa na Diamondni ishara ya yeye kuonyesha kuwa anakubali kuwa nabii issa kasulubiwa, sasa si bora hatuambie kuwa yeye sio muislamu, kwanini uwaambie watu kuwa wewe ni muislamu alafu  unavaaa msalaba, na katika nyimbo zake  si bora angeimba nimbo nyinyine nyingine tu, anaimba Halleluyah”.

Halleluyah ni moja ya nyimbo mpya za Diamond ambazo zinafanya vizuri duniani kote, wimbo huo uliotoka mwezi uliopita amewashirikisha kundi la muziki la MorganHeritage.

Ikiwa kama nyimbo mojawapo iliyomfanya   Diamond aendele kujulikana kimataifa na  anaona alipiga hatua kubwa katika muziki kutokana na kushirikiana na wanamuziki wakubwa Duniani, Diamond aliimba wimbo huo kwa dhumuni la kikidhi mahitaji ya mashabiki.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa msanii Diamond  na wasanii wengine kuongelewa na viongozi wa dini zao  kutokana na nyimbo wanazoimba, lakini kwa upande wa Diamond  haijawa wazi kuwa mambo hayo yote ambayo Diamond amefanya katika wimbo huo alimaanisha  kile ambacho viongozi wa dini watakuwa wamekimahanisha pia.

Bado diamond hajajibu chochote kuhusu tuhuma hizo alizoshtakiwa na viongozi wa dini yake, lakini nadhani inampasa kujibu ili aweze kuweka wazi kwa watu pia.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *