Viongozi wa Kikanda kutoka Afrika Mashariki wanatarajia kukutana katika kikao cha dharura jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili mzozo unaondelea Sudan Kusini.

South Sudan

Marais hao kutoka mataifa wanachama wa IGAD watajadili kwa kina pendekezo la Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika AU kutaka kutuma vikosi vya usalama baada ya kuzuka upya kwa mapigano kati ya majeshi ya serikali na vikosi vya aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.

Hayo yanajiri siku mbili tu baada ya Rais Salva Kiir kuwatimua kazi mawaziri, washauri na wabunge wote wanaoegemea mrengo wa Machar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *