Waigizaji nyota wa filamu za ‘Fast and Furious’ Vin Diesel na The Rock wamemaliza tofauti zao zilizodumu kwa muda mrefu kati ya wawili hao.

Vin Diesel ambaye mapema mwezi uliopita alinukuliwa akisema kuwa hata katika maisha ya kawaida hawezi kupigwa na The Rock.

Kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya ‘The Rock’, alituma ujumbe ambao uliashiria kuwa  wawili hao wameshamaliza bifu lao na wameruhusu maisha yao kusonga kama zamani.

Vin Diesel aliposti picha akiwa na The Rock kwenye ukurasa wake wa Instagram akimtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa kwa kuandika “Nikitazama ni mangapi tumeyafanya, Ni mangapi tumeshikana bega kwa bega ili kufanikisha hata yale yasiyowezekana,Najivunia sana kuwa na wewe.”

Aliongeza kwa kuandika  “Tuko poa, tunapendana,Ni jamaa wangu wa karibu muda wote ,vilikuwa ni vitu vidogo tuu“.

Kwenye posti hiyo Vin Diesel ameendelea kusisitiza kuwa sio tu wawili hao wanaishia kuonana location bali muda mwingine hutembeleana kwenye familia zao.

Wawili hao waliingia kwenye bifu kali mwaka jana wakati wa utengenezaji wa Fast 8,ambapo inasemekana kuwa wawili hao walizichapa wakiwa location.

.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *