Vijana wawili wamekamatwa baada ya kumfanyia kampeni mgombea urais nchini Marekani, Donald Trump katika ubalozi wa Marekani mjini Kampala nchini Uganda.

Wafuasi hao wa Trump waliambiwa na maafisa wa polisi kwamba hawataruhusiwa ndani ya ubalozi kwa sababu walikuwa hawajapata rukhusa.

Mtandao unaounga mkono serikali Chimp Riports umesema kuwa Vijana hao wa kundi la Young Democrats nchini humo walijaribu kuingia katika ubalozi wa Marekani.

Gazeti la Daily Monitor limechapisha ujumbe wa Twitter likionyesha picha za waandamanaji hao.

Trump katika ilani yake ya uchaguzi amesema kuwa atakabiliana na marais waliohudumu kwa muda mrefu kutoka Afrika akiwemo rais Museveni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *