Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imefuta kesi iliyokuwa inawakabili vijana saba wa Chama Cha Demeokrsai na Maendeleo (CHADEMA).

Vijana hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya ukusanyaji matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Hatua hii imekuja baada ya upande wa mashitaka kuliondoa shauri hili mahakamani kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kifungu cha 91(1).

Washitakiwa wote saba wameachiwa huru na Mahakama hiyo kuanzia leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *