Aliyekuwa mshiriki wa miss Tanzania mwaka 2003, Nargis Mohamed ameamua kuandaa mafunzo maalum ya fani ya urembo nchini.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar e saalam, Nargis Mohamed ambaye alishika nafasi ya tatu kwenye mashindano ya miss Tanzania mwaka huo amesema kuwa ameamua kuandaa mafunzo hayo kwa ajili ya wanawake  na vijana wanaopenda kujifunza fani hiyo.

Mrembo huyo amesema kuwa “Mafunzo hayo hayachagui jinsia, nia yeti kubwa sisi ni kuwawezesha wenzetu kwa kuwapa ujuzi ili waweze kujiinua kiuchumi kama wajasiliamali na kujijenga kimaisha sambamba na mpango wa serikali yetu kujenga ajira na kujikwamua kutoka kwenye umaskini,”.

Nargis Mohamed aliyepata umaarufu kupitia video ya Profesa Jay, Zari la Mentali amesema kuwa mafunzo hayo yanapatikana kwa bei nafuu kabisa kupitia tovuti ya www.glammadamlive.com, na wataosajiliwa wataweza kufanya malipo kupitia Vodacom M-pesa na Tigo Pesa.

Kwa wale walio nje ya nchi wanaweza kutumia kadi tofauti kama VISA, MasterCard, American Express ili kufanikisha zoezi hilo.

Pia amesema kuwa gharama ya mafunzo hayo ni shillingi elfu 10 za kwa mwezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *