Video queen alietumika katika wimbo wa Harmonize ‘sheri’ Tahiya amekanusha kutoka kimapenzi na Diamond huku kusema kuwa yeye na Diamond hawana mahusiano yoyote zaidi ya kazi.

Mwanadada huyo ambae amekuwa akionekana kuwa karibu na wasanii kutoka Wcb amesema kwa yeye kuonekana karibu na wasanii hao ni kitu kusichokwepeka kwa sababu kazi zake zinamfanya awe nao karibu kila muda.Hata hivyo dada huyo alisema kuwa yeye na Diamondi ni ndugu.

‘Mimi na diamond ni ndugu, sio ndugu wa karibu sana ila kupitia Esma, so ikitokea shughuli shughuli zake,party zake na events mimi ninakuwa ni mmoja kati ya watu wanaosapoti kazi hizo, so mimi kuwa karibu  nae recently ni kwa sababu ya yeye na  birthday zake kufululiza,birthday tano alifanya na zote nilikuwepo kuanzia ya kwanza hadi ya mwisho.

Hata hivyo aliendelea kuelezea pia ni kwa sababu gani,watu walianza kumzushia kuwa anatembea nae,”katika birthday tulikuwa tunasnap na vitu kama hivyo, waking up nakutana na post kuwa katika birthday yake ya mwisho niliondoka nae nikaenda kulala nae nyumbani kwake,na kwamba ile snap ya Diamond karanga pale kitandani ni kitandani kwake na ule mkono wa mamangu ni mkono wake,…lakini nobody knows the truth zaidi ya sisi hapa”.

Imekuwa ni gumzo mitandaoni kuwa karibia kila msichana ambae anaonekana kuwa karibu na msanii huyo kwa sasa basi anakuwa nae katika uhusiano wa kimapenzi labda kutokana na kile kilichotokea kwa video queen Hamisa Mobeto hivyo mashabiki wa Diamond wamepoteza uaminifu kwa msanii wao.

Hata hivyo baadhi ya mambo yanakuwa yanakuzwa sana katika  mitandao ya kijamii, mwanadada Tahiya anasema kuwa kitendo cha yeye   kupost snap ile wakati maneno ya yeye kutembea na msanii huyo yanendelea kumeafanya katika mitandao kuzidi kuchafuka kuwa anatembea nae lakini ukweli wanaujua wao wawili kuwa hakuna kitu chochote kinachoendelea zaidi ya kuwa katika kazi pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *