Ni mashindano yanayofanywa mara kwa mara na wasanii wa muziki wa rap katika kuonyesha na uwezo na vipaji vya kutunga na kuimba papo kwa hapo.

Hii ni free style, ambayo mwa mastaa wengi wa Hip Hop huamini ndio kipimo halisi cha kumpata Natural Rapper au The Most Talented Hip Hop Rappers.

Hii ndio footage ya Harmorapa akimuonyesha MAUJUZI Rapper Harmorapa amekutana uso kwa uso na msanii mkongwe wa muziki wa hip hip ambaye pia ni mbunge wa Mikumi Joseph Haule aka Professor Jay na kumuonyesha mkongwe huyo kile anachokifanya kwenye muziki wa hip hop.

Wawili hao walikutana wiki iliyopita katika studio ya Parazobeats ya producer Mr Ttouch iliyopo Sinza Parestina jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa video hiyo, Mr T touch alimuamuru Harmorapa kuchana kidogo ili Professor Jay aone kipaji cha kijana huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *