Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Barnaba kupitia akaunti yake ya Instagram ametoa taarifa ya kuibiwa vitu vyake ndani ya gari lake usiku wa kuamkia leo.

Barnaba ameandika kwenye ukurasa wake wa instagramu kuwa ameibiwa begi dogo ambalo ndani yake kulikuwa na ‘Laptop’ mbili za aina ya ‘Mac’ moja Pro X Letina(Kompyuta mpakato), External mbili, faili lake lenye mikataba mbalimbali pamoja na hati ya kusafiria ‘Passport’.

Baranaba ameandika Naomba sana sana waungwana kama kuna mtu yotote atabaini au kujua vilipo au hata kupelekewa basi naomba wasamalia wema mnirudishie au kuniletea  napatikana kwa ‘No 0743505010’ Mungu awabariki  naamini aliyenavyo hajaiba bali amepitiwa katika njia ya kutafuta riziki nami kwa jina la Mungu nitamsamehe na nimesamehe ila kama ana rohoo nzuri na ameguswa basi naomba waungwana mnipigie hata kama umeokota”

Barbana ambaye anatamba na wimbo wake  ‘Lonely’ ameelezea tukio hilo ka kusema kuwa limetokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *