Mkali wa ‘Cash Madame’ Vanessa Mdee anatarajia kuonekana kwenye tamthilia ya Shuga iliyochezwa nchini Afrika Kusini kuanzia mwakani.

Msimu wa tano wa tamthilia hiyo unaanza Machi mwakani ambapo Vanessa Mdee kutokaatashirikiana na wasanii wengine kutoka nchi mbalimbali katika kunogesha msimu huo wa tamthilia hiyo.

Vanessa Mdee amesema kuwa “Nafurahi mwaka huu naumaliza vizuri na wimbo wangu wa ‘Cashmadame’ lakini mwakani Mungu akipenda nitauanza tena vyema kwa kuwa nimechaguliwa na MTV Base nishiriki katika tamthilia ya Shuga kwa msimu wa tano, ni mafanikio makubwa kwangu na kwa taifa langu na hii ndiyo itakuwa tamthilia yangu ya kwanza kuwahi kuigiza,”.

Tamthilia hiyo anayokwenda kushiriki Vanessa ina umaarufu mkubwa kutokana na watu wengi maarufu kuwahi kushiriki akiwamo mshindi wa tuzo ya Oscar mwaka 2014, Lupita Nyong’o kupitia filamu ya ‘Twelve Years a Slave’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *