Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amefunguka kwa kusema kuwa bado anampenda na ataendelea kumpenda aliyekuwa mpenzii wake Jux ambaye hivi karibuni wameweka wazi kuvunjika kwa mahusiano yao.

Pia ameeleza kuwa wimbo wa kisela ni wimbo ambao asilimia kubwa ni ukweli mtupu kuhusu  maisha halisi ya kimapenzi kati yake na aliyekuwa mpenzi wake Jux.

Vanessa amesema kuwa ”Everything ambacho kimeandikwa kwenye kisela ni ukweli mtupu, unajua kuna tabia za kisela lakini mapenzi sio ya kisela” amesema Vanessa.

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa kuwa  alirekodi wimbo wa Kisela akiwa analia kutokana huzuni kubwa aliyokuwa nayo moyoni kipindi hicho.

Vanessa na Jux walikuwa wapenzi kwa miaka kadhaa kabla ya wawili hao kuachana hivi karibu kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri kama zamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *