Mwanamuziki wa Bongo fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amechaguliwa kuwania tuzo za MTV MAMA katika kipengele cha msanii bora wa kike Afrika zitakazofanyika jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Vee Money ambaye anaiwakikisha  vizuri Tanzania katika anga za mziki kimataifa, kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost picha zinazoonyesha kuchaguliwa kuwania tuzo  hizo.

Vee alipost na  kuishukuru MTVAfrica  kwa nafasi hiyo ya kipee  ya kuwa kati ya wasanii watano bora barani  Afrika.

Mbali na Vee Money wasanii wengine wanaowania tuzo hizo kutoka Tanzania ni Diamond Platnumz, Alikiba pamoja na Navy Kenzo.

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Oktoba 22 katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *