Mwanamuziki nyota anayefanya vizuri kwasasa, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amesema anajisikia furaha kuwemo kwenye kinyang’anyiro cha mwanamuziki bora wa kike kwenye Tuzo za EATV.

Mwanamuziki huyo yupo kwenye kipengere cha mwanamuziki bora wa kike akichauana wasanii wenzake kama vile Lady Jay Dee, Linah, Lilian Mbabazi pamoja na Ruby.

Vanessa Mdee amesema kipengele hicho ni kigumu sana kwake kutokana na wasanii wengine wa kike waliopo kuwa na uwezo mkubwa, hivyo imekuwa changamoto kubwa kwake.

Pia Vanessa Mdee amesema anautamani sana usiku wa EATV AWARDS, ili kuweza kukutana na wasanii wenzake ambao mara nyingi amekuwa akikosa muda wa kuonana nao pamoja na wadau wa muziki  lakini kikubwa tayari amesha andaa hadi vazi la kuvaa siku hiyo.

Mwanamuziki huyo alikuwemo kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za MTV MAMA zilizofanyika Oktoba 20 nchini Afrika Kusini katika kipengere cha mwanamuziki bora wa kike ambapo Yemi Alade aliibuka mshindi.

Tuzo za EATV zimeandaliwa na kituo cha runinga cha EATV na kushirikisha wanamuziki kutoka ukanda wa Afrika Mashariki ambapo zitafanyika Desemba 10 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *