Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa tuhumu za kujihusisha na biashara za dawa za kulevya.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Simon Sirro amesema msanii huyo alikamatwa juzi na wanaendelea na mahojiano ili kubaini kama wanajihusisha na biashara hiyo au la.

Sirro aliwaomba wananchi, kuendelea kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na biashara hiyo, lengo likiwa ni kuhakikisha suala la dawa za kulevya linamalizwa katika mkoa huo.

Mwezi uliopita msanii Vanessa alitajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa anasadikiwa kujihusisha na biashara hiyo, ambapo alitakiwa kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda hiyo kwa mahojiano, lakini alishindwa kufika kutokana na kuwepo nchini Afrika Kusini kikazi.

Taarifa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, zinasema msanii huyo alijisalimisha katika kituo hicho juzi ; na polisi walimpekua nyumbani kwake, kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *