Staa wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee a.k.a Cash Madame nae amevunja ukimya kuhusiana na sakata la ‘unga’ la Mh. Paul Makonda.

Staa huyo mwenye uhusaino wa kimapenzi na staa mwenzake, Jux alitajwa siku chache baada mastaa wengine kutajwa kuhusika na sakata la unga kwa namna tofauti ikiwemo uuzaji, usambazaji na utumiaji.

Vee Money mwenye mkataba wa kuigiza filamu ya SHUGA nchini Afrika Kusini alikosakana wakati wenzake waliporipoti kituo kikuu cha polisi.

Baada ya sakata hilo, Cash Madame nae ameamua kufungukia sakata hilo.

Akiwa anaonekana kwenye harakati za ku-shoot nchini Afrika Kusini, Vee Money ameandika: ‘The show must go on … bomb ass dress from @asos #FILA’.

Kisha akaandika: ‘The night is darkest before the dawn. #Breakthrough #Juu #CashMadame #SheKing.’

Haijajulikana siku ambayo Vee Money atarejea nchini kwaajili ya kuhojiwa na jeshi la polisi nchini kama ilivyotokea kwa mastaa wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *