Beki wa kulia wa Manchester United, Antonio Valencia ameongeza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu hiyo ambapo atabakia Old Traford mpaka mwisho wa msimu wa mwaka 2018.

Valencia amecheza mechi 271 na kushinda magoli 21 na amenikiwa kutwaa mataji sita toka ajiunge na klabu hiyo akitokea Wigan Athletic mwaka 2009.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka wa miaka 31 amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Manchester United chini kocha Jose Mourinho baada ya kucheza mechi 23 katika mashindano mbali mbali.

Hadi sasa hivi Valencia ana miaka minane toka ajiunge Manchester United ambapo amesajiliwa na kocha wa wakati huo, Sir Alex Furguson mwaka 2009.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *