Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umemtaka mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Edward Lowassa kuacha uongo kwani hana historia ya kupigania maslahi ya umma.

UVCCM wamesema kuwa madai ya lowassa kwamba aliwahidi wananchi angeunda Tume ya kupitia mikataba ya madini kama angeshinda urais ni uongo na kutaka kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

Pia umoja huo umemtaka Lowassa kuonyesha ushahidi video ya matamshi yake wakati akiwa katika mkutano wa hadhara akihutubia mkoani Geita ikionyeaha kama kweli alitoa matamshi hayo.

Hayo yalielezwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipozumgumza waandishi wa habari jana ofisini kwake Upanga jijini Dar Es Salam.

Amesema Lowassa hama nguvu za uzalendo wa kupigania au kuzungumzia mapambano dhidi ya ubadhirifu wa mali za umma kwasababu hata kujiuzulu kwake kulitokana na shinikizo la bunge huku akihusishwa na sakata la ufisadi.

Shaka alibainisha kuwa hakuna ushahidi wala kumbukumbu inayoonyesha kuwa Lowasa siku moja aliwahi kutetea maslahi ya umma wakati akiwa serikalini kama Waziri au alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

Shaka amesema kama kweli angekuwa na ujasiri huo wakati alipokuwa waziri mkuu angeweza kutamka maneno hayo au kumshauri Rais iundwe Tume lakini alishindwa kwa sababu hana ujasiri na uzalendo kama anavyotaka kuwaaminisha wananchi baada ya kuona Rais John Magufuli akiungwa mkono kitaifa na kimataifa.

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *