Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewateua maofisa sita wa uhamiaji kushika nyadhifa mbalimbali katika jeshi hilo.

Wateule hao ni Mrakibu wa Uhamiaji (SI) Edward Peter Chogero kuwa Kamishna wa Divisheni ya Fedha na Utawala, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Samwel Rhobby Magweiga kuwa Kamishna wa Makamishna Divisheni ya Udhibiti na Uongozi wa Mipaka.

Wengine ni Mrakibu Mwandamizi (SSI) wa Uhamiaji Gerald John Kihinga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Pasipoti na Uraia, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Musanga Mbusuro Etimba ambaye anakuwa Kamishna wa Divisheni ya Hati za Ukaazi na Pasi.

Aidha Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Hennerole Morgan Manyanga ameteuliwa kuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria.

Rais amemteua pia Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mourice David Kitinusa kuwa Kamishna Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *