Kifo cha mwanamuziki wa Uingereza, Michael George aliyefariki siku ya Krismasi bado hakijaelezwa nini chanzo cha kifo cha mwanamuziki huyo.

Baada ya kifo hicho rafiki wa karibu wa mwanamuziki huyo aitwaye Fadi Fawazi amesema kuwa alimkuta rafiki yake huyo akiwa huku akiwa amelala kitandani nyumbani kwake.

Kutokana na kifo hicho rafiki yake huyo ameandika ujumbe kutia akaunti yake ya Twita kwamba “Ni Krismasi, sitasahau kumkuta mshikaji wangu amefariki kwa amani kitandani mapema asubuhi.  Daima nitakukumbuka XX.”

Madaktari waliofika kwenye makazi ya mwanamuziki huyo baada ya mwili wake kugunduliwa, walihisi mwanamuziki huyo amefariki kwa ugonjwa wa moyo.

Polisi bado wanaendelea na uchunguza kuona iwapo kuna tendo la jinai lilifanyika katika kifo chake, japokuwa hadi sasa hapajaonekana kitu chochote.

Pamoja na yote hayo, Fadi hajahojiwa chochote kama mtuhumiwa katika kifo hicho.  Watu hao wamekuwa wakishirikiana tangu walipoonekana pamoja huko Venice, Italia.
Mwanamuziki huyo ambaye jina lake, Georgios Kyriacos Panayiotou aliteka mioyo ya watu kutokana na nyimbo zake kuwa bora.

Katika miaka ya karibuni alikuwa akikabiliwa na tatizo la madawa ya kulevya na kukamatwa kila mara kwa makosa mbalimbali ya uvunjaji wa sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *