Mwanamuziki nyota anayefanya vizuri kwasasa Baraka The Prince amesema hakupendezewa na mchekeshaji, Stan Bakora alivyofanya cover ya niymbo yake ‘Nisamehe’ aliyomshirikisha Alikiba.

Stan Bakora ametoa video ya wimbo huo ikimuonesha amejipakaa mkaa akimaanisha weusi wa Baraka The Prince kitu ambacho mwanamuziki huyo akupendezewa nacho mpaka kupelekea kuandika maneno kwenye akaunti yake ya Instagram.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Baraka The Prince ameandika ‘Matani ni mazuri ila yakizidi yanaweza kuleta matatizo… heshima ichukue nafasi yake tafadhali mzee utani huu sijaupenda iwe mwanzo na mwisho tafadhali‘.

Kwa upande wake Stan Bakora amesema kuwa kabla ajafanya cover ya mwanamuziki yeyote ni lazima azungumze naye akikubali ndiyo hufanya kwa hiyo alishakubaliana na Baraka lakini anashangaa mwanamuziki huyo anapaniki.

Stan Bakora ni mchekeshaji aliyejizolea umaarufu kupitia sanaa ya uchekeshaji baada ya kufanya kwenye vichekesho vya mkude simba vinavyoendelea kufanya vizuri hadi sasa.

 

                                                                                 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *