Liverpool na Everton leo zitakutana kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza msimu huu katika uwanja wa Goodson Park.

Mechi ya mwisho baina ya klabu hizo msimu uliopita Liverpool ilishinda 4-0 katika uwanja wa Anfield Aprili 20 mwaka huu.

Mambo muhimu katika mchezo huo

Liverpool ameshinda mechi 89 dhidi ya  66 za Everton unawafanya kuwa wababe zaidi ya Everton huku mechi 71 zikimalizika kwa sare.

Straika wa zamani wa Liverpool, Ian Rush ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao mengi kwenye mechi hiyo hii ambapo alitupia jumla ya mabao 25, 13 kati ya hayo yakiwa ni katika ligi.

Aliyekuwa golikipa wa Everton Neville Southall anashikilia rekodi ya kucheza mechi 40 kati ya mwaka 1981 na 1998.

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez ndiye mchezaji aliyefunga goli bora katika mechi ya watani wa jadi hao alipoifungia Liverpool goli la faulo mwaka 2013.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *