Mwanamuziki wa Marekani, Usher Raymond yupo hapa nchini akitembelea eneo la uhifadhi wa wanyama pori la Serengti National Park.

Raymond aliweka baadhi ya picha akiwa na familia yake katika akaunti yake ya Twitter na kujulisha kuwa Serengeti na familia yake.

Mwanamuziki kwenye picha hiyo ameelezea hali ilivyo katika eneo hilo ambapo nni mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara.

Watu wengine maarufu akiwemo mchezaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid David Becham, aliyekuwa mchezaji wa Liverpool Mamadou Sakho, mchezaji wa Everton Morgan Schneiderlin ni miongoni mwa wale waliozuri katika sehemu mbali mbali za kitalii nchini mwaka huu.

Vivutio vya kitalii nchini Tanzania kama vile mbunga ya uhifadhi wa wanyama pori ya Serengeti na mlima Kilimanjaro ni vivutio vinavyoongoza kwa utalii ambapo watu wengi maarufu wametembelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *