Mwanamuzi maarufu wa R&B nchini Marekani, Usher Raymond amepewa tuzo ya Heshima ya Hollywood Walk of Fame.

Tuzo hiyo imetokana na mafanikio, mchango na ushawishi wake kwenye muziki nchini Marekani na duniani kwa ujumla.

Staa huyo pia ametengenezewa Nyota kubwa ya jina lake kitu ambacho mastaa wachache sana wanafanyiwa kutokana na hadhi yao pamoja na mchango wake katika muziki na jamii kwa ujumla ambapo Usher amefanikiwa kufanya vitu hivyo.

Usher Raymond ni mwanamuziki mkongwe katika nchi ya Marekani kutokana na kuanza muziki miaka ya tisini ambapo hadi leo bado anafanya vizuri katika suala zima la uimbaji ambapo vibao vyake vinabamba duniani kote.

Usher pia ndiye aliyegundua kipaji cha mwanamuzi Justin Bieber ambaye kwasasa ni mwanamuziki bora duniani kote baada ya kutolewa kimuziki na Usher Raymond.

Baadhi ya nyimbo alizowahi kutamba nazo Usher Raymond ni My Boo, I don’t Mind, U Got It Bad, No Limit na nyingine kibao pia aliwahi kushirikishwa kwenye nyimbo kama I need Girl ya Diddy ambapo aliimba kiitikio kwenye nyimbo hiyo na kufanya watu kumjua zaidi.

Usher Raymond ni mwanamuziki, mtunzi, muigizaji wa filamu na mchezaji (Dancer) amezaliwa mwaka 1974 katika mji wa Dallas, Texas nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *