Rais wa FIFA, Gianni Infantino ameeleza kuwa Lionel Messi anatakiwa ashinde kombe la dunia ili awe mchezaji bora wa muda wote katika historia ya soka.

Amesema Messi ni mchezaji mzuri lakini hawezi kuwa mchezaji bora wa muda wote mpaka ashinde kombe la Dunia.

“Messi ni mchezaji wa kiwango cha juu lakini hajashinda ubingwa wa dunia akiwa na timu yake ya taifa hivyo anakosa sifa moja maana kuna wachezaji wengi tu wazuri hawajawahi kushinda kombe la dunia na hiyo ndio tofauti yao na Maradona”,.

Messi na timu yake ya Argentina ipo kwenye mtihani wa kufuzu au kukosa fainali za kombe la dunia 2018 nchini Urusi ambapo alfajiri ya kesho wanahitaji kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu au kucheza Play off na timu ya taifa ya New Zealand.

Infantino ameongeza kuwa Messi ana uwezo wa kucheza fainali za mwaka 2022 endapo ataendelea kujitunza kama sasa hivi ambapo hapati majeruhi ya mara kwa mara.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *