Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bill Nass amewataka Roma Mkatoliki na wenzie ambao walikumbwa na mkasa wa kutekwa kutokuwa na mawazo kuhusu sakata hilo badala yake waendelee na kazi zao.

Kauli hiyo ya Bill Nass imekuja kufuatia maneno ya watu katika mitandao ya kijamii kwa kusema kuwa Roma na wenzie wameshindwa kueleza ukweli juu ya suala lao la kutekwa.

Bill Nass amewataka Roma na wenzie kuendelea na maisha kwa kufanya kazi ingawa hawatokuwa vizuri lakini kwa sababu wana uhai na uzima katika maisha yao wanapaswa kumshukuru Mungu.

”Wanapaswa kumshukuru Mungu kwa kuwa wako hai. Wendelee kufanya kazi kwa moyo, japo unapokuwa na pressure huwezi kufanya. Kwa mfano, mimi tu nikiwa hivyo mood za studio zinakata. Japo wao wanaweza kuwa zaidi ya hapo, ila hizo ni changamoto tu, so, isiwafanye wakaishia hapo as long as wako hai na wazima.”.

Roma na wenzake watatu akiwemo Moni Cntre Zone walitekwa na watu wasiojulikana wakati wakiwa studio za Tongwe Records zilizopo maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *