Ingawa ni vigumu sana kuamini kuwa hii ni mojawapo wa nyenzo za kuutangaza muziki au biashara inayoshabihiana na muziki duniani lakini hali hii imeendela kuwepo karibu kila siku na kila mahali.

Wasanii wengi hasa chipukizi au wasanii ambao wana hadhi mbele ya jamii lakini kwakua walikuwa wamepotea kwenye macho na masikio ya mashabiki kwa muda mrefu pindi wanapotaka kuachia kazi mpya huanza kutenegeneza muonekano wao kwa njia mbaya kabla ya kuachia kazi hizo.

Hivi karibuni msanii wa WCB, Raymond aliachia ngoma yake ya pili tangu jiunge na lebo hiyo iitwayo NATAFUTA KIKI lakini kama hiyo haijawastua wasanii kuelewa kuwa wanayoyafanya hayawasaidii leo tena, kambi ya Mkubwa na Wanawake kupitia kwa kiongozi wa Yamoto Band, Asley Isihaka maarufu kama DOGO ASLEY imekumbwa tena na tatizo hilo hilo.

Ingawa bado haijathibitika kuwa ni tatizo lakini dalili ya mvua ni mawingu na waswahili husema LISEMWALO LIPO NA KAMA HALIPO BASI LAJA………From NOWHERE Asley na ataa mwingine wa kike Ruby wameibuka na kuanza kudai kuwa wao ni wapenzi (tena ) walio kwenye mahaba mazito mno.

Halafu punde si punde ngoma mpya ya YAMOTO BAND wakimshirikisha Ruby ‘SUU’ unaachiwa hewani na miongoni mwa viashiria kuwa wawili hao WANAIGIZA ni matumizi ya neno SUU kwenye ujumbe zao zilizopo kwenye mitandao ya kijamii.

Je, mastaa hawa nao WANATAFUTA KIKI au HAWAELEWI ATHARI YA JAMBO HILO?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *