Vilabu vya soka barani ulaya vimefanya usajili wa kumarisha vikosi vyao katika siku ya mwisho ya usajili uliofungwa usiku wa kuamkia Septemba mosi.

Chelsea wamemrejesha beki wao kisiki David Luiz waliomuuza miaka miwili iliyopita kwa Paris St- Germain, mchezaji huyu kanunuliwa kwa kiasi cha pauni million 34.

Pia Chelsea imemsajili Marcos Alonso toka Fiorentina kwa pauni milion 23.

Moussa Sissoko amesajiliwa na Tottenham akitokea Newcastle kwa pauni milioni 30 na Leicester City wamesajili Islam Slimani toka Sporting Lisbon kwa pauni 29.

Stoke City wamemsajili Wilfried Bony kwa mkopo toka Manchester City, Samir Nasri nae amepelekwa kwa mkopo Sevilla toka kwa matajiri wa Man City

Mshambuliaji Mario Balotelli wa Liverpool amesajiliwa na Nice ya Ufaransa bure, West Ham wamsajili beki Alvaro Arbeloa toka Real Madrid.

Valencia ya Hispania wamesamjili kwa mkopo wa muda mrefu Eliaquim Mangala wa Manchester City, Nao Juventus wamemsajili Juan Cuadrado kwa mkopo toka Chelsea kwa mkataba wa miaka mitatu.

Jack Wilshere ametua Bournemouth kwa mkopo wa msimu mzima, Mshambuliaji Mkongo Dieumerci Mbokani asajiliwa na Hull City.

Enner Valencia aenda Everton kwa mkopo hadi mwisho wa msimu kutoka West Ham.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *