Nchi ya Urusi imesema kuwa itaanza kupunguza wanajeshi wake nchini Syria na itaanza kwa kupunguza meli zake zenye uwezo wa kubeba ndege za kivita.

Kwa mujibu wa mkuu wa majeshi ya Urusi, Andrei Kartapolov amesema kuwa hatua inakuja baada ya Urusi na Uturuki kufanikisha kupatikana na makubaliano ya kusitisha vita.

Urusi imekuwa ikitekeleza mashambulio ya kutoka angani dhidi ya waasi wanaoipinga serikali tangu 2015.

Kushiriki kwa Urusi katika vita hivyo kulimsaidia sana mshirika wake, Rais wa Syria Bashar al-Assad ambaye amegoma kuachia madaraka mpaka kusababisha mauaji makubwa nchini humo..

Kamanda wa majeshi ya Urusi nchini Syria Kanali Jenerali Andrei Kartapolov amenukuliwa akisema majukumu yaliyotengewa meli kubwa ya kubeba ndege za kivita ya Admiral Kuznetsov yamekamilishwa.

Urusi ilitekeleza mashambulio ya kwanza ya angani Syria Septemba 2015, ambapo ilisema ililenga wapiganaji wa Islamic State.

Mwezi Machi, ilitangaza ingeanza kuondoa baadhi ya wanajeshi wake lakini ikaendelea kutekeleza mashambulio ya angani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *