Michuano ya kombe la mabara itaendelea tena leo hii kwa michezo miwili ya kundi A kuchezwa, wenyeji Urusi watashuka katika dimba la Otkrytiye Mjini Moscow, kucheza na Ureno.

Mwamuzi Gianluca Rocchi kutoka Italia ndie atakae chezesha mchezo huo wa wenyeji na Ureno na mchezo huo utacheza saa kumi na mbili jioni kwa saa za Afrika mashariki.

Na mchezo wa pili wawakilishi wa bara la Afrika katika michuano hiyo timu ya Cameroon watashuka katika dimba la Fisht Olympic kupepetana na New Zealand , mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi Bakary Gassama kutoka Gambia.

Urusi ndio vinara wa kundi A wakiwa na alama tatu baada ya kupata ushindi dhidi ya New Zealand, Ureno na Cameroon wao wana alama moja moja na New Zealand wanaburuza mkia wakiwa hawana alama hata moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *