Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa urais nchini Gambia yanaonesha mgombea wa upanzani Adama Barrow kushinda dhidi ya Rais Yahya Jammeh.

Matokeo hayo yanaonesha mpinzani huyo kushinda katika mji mkuu wa nchi hiyo Banjul kutokana na matokeo ya awali.

Hata hivyo ni chini ya asilimia 15 ya karibu wapiga kura 890,000 waliosajiliwa ndio imehesabiwa.

Wanajeshi na polisi leo wameweka vituo vya ukaguzi kwenye barabara zinazoingia na kutoka mji mkuu.

Serika ilizima huduma za mitandao na kufunga simu za kimataifa wakati uchaguzi ukuwa unaendelea.

Jammeh ameitawala Gambia tangu mwaka 1994 kufuatia mapinduzi ya kijeshi na sasa anawania muhula wa tano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *