Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amesema hawezi kuachia ngoma yake mpya kama jinsi ambavyo alivyokuwa amepanga kutokana na watanzania wengi kuwa ‘busy’ na masuala ya siasa.

Janjaro amedai anafanya muziki wa biashara hivyo haoni sababu ya kutoa kazi mpya katika kipindi ambacho upepo wa kibiashara haujamnyookea.

Hata hivyo Janjaro ameongeza kuwa hana haraka ya kuachia wimbo mpya tofauti na wakongwe wanavyopata ‘presha’ kwa sababu bado anadhani ana miaka mingi katika soko la muziki.

Mbali na Janjaro upepo huu wa siasa pia ulimkumba msanii mkongwe Jay Moe ambaye amelazimika kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Nisaidie Kushare‘ wiki iliyopita baada ya kushindwa kuutoa tangu mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa kuhofia kufunikwa na kiki za siasa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *