Jeshi la Polisi nchini limesema linaendelea na upelelezi wa miili 7 ya watu iliyokutwa ikielea katika mto Ruvu wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ili kutambua chanzo cha vifo vya marehemu hao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Kamishna wa Polisi, Robert Boaz wakati akiongea na waandishi wa habari.

Kamishna Boaz amesema jeshi hilo bado halijawatambua marehemu hao hadi sasa huku akitetea uamuzi wa jeshi hilo kuzika haraka miili ya marehemu 6 kati ya 7.

Amesema jeshi hilo lilipata taarifa za kuelea kwa maiti 7 katika mto Ruvu eneo la Makurunge wilayani Bagamoyo kati ya tarehe 6/12/2016 hadi 9/12/2016 ambapo askari na daktari walifika katika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa kitaalam.

Pia aliongeza kwa kusema miili 6 kati ya 7 ilikuwa imeharibika sana na ndiyo maana iliamuliwa zizikwe katika eneo la tukio wakati moja yenye unafuu ikipelekwa hospitali ya wilaya ya Bagamoyo hadi tarehe 16/12/2016 ilipozikwa na halmashauri baada ya kutotambuliwa na tu yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *