Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi wa kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili video queen, Agnes Gerald maarufu kama Masogange bado haujakamilika.

Kesi ya Masogane imekuja leo kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri lakini wakati kesi hiyo ikiharishwa Masogange alikuwa ajawasili mahakamani hapo.

Wakili wa Serikali Adolf Mkini amesema kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika na mshtakiwa hakufika mahakamani hapo.

Kabla ya upande wa Serikali haujasema kitu Wakili wa Masogange, Nictogen Itege aliwasilisha udhuru wa mteja wake kutokuwepo mahakamani hapo.

Kutokana na hayo Hakimu Mashauri alimtaka mshatakiwa kuheshimu masharti ya mahakama.

Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroine na Oxazepam.

Kesi hiyo imehairishwa mpaka Aprili 20 mwaka huu itakapotajwa tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *