Upasuaji wa kwanza wa kushuka kokwa za korodani za mtoto wa miaka nane ambazo hazikushuka kama inavyotakiwa umefanyika kwa mafanikio chini ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Upasuaji huo umefanywa kwa kutumia njia ya matundu madogo (Laparoscopic surgery) kwa ushirikiano wa madaktari wa MNH na wa Hospitali ya King Faisal ya Saudi Arabia.

Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto, Zaituni Bokhary amesema upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio makubwa.

Daktari huyo amesema kokwa za kiume zinapaswa kushuka na kukaa katika vifuko vya korodani na kwamba iwapo zitaendelea kubakia tumboni husababisha tatizo la kushindwa kutungisha mimba.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa pamoja na mtoto huyo, pia wamefanikiwa kuwafanyia upasuaji kwa watoto wengine waliokuwa na matatizo mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *