Kiungo wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Arsenal, Santi Cazorla anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu kutokana na jerahaa la kiundo cha mguu.

 

Kiungo huyo atafanyiwa upasuaji katika kifundo cha mguu wake wa kulia na hivyo atakaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu.

 

Cazorla ambaye aliumia katika ushindi wa 6-0 wa mechi ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Ludogorets kwenye uwanja wa Emirates Oktoba 19 mwaka huu.

Arsenal wamesema kuwa mchezaji huyo atasafiri wiki ijayo kuelekea nchini Sweden kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji huo wa kifundo chake.

Mbali na Cazola kuwamajeruhi wachezaji wengine wa klabu hiyo walio majeruhi ni Debuchy, Giroud pamoja na Hectort Bellerin.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *