Umoja wa Mataifa (UN) umelaani vikali mauaji ya wafanyakazi sita wa kutoa misaada nchini Sudan Kusini.

Miongoni mwa waliouawa ni raia watatu kutoka Kenya, na watatu kutoka Sudan Kusini ambao walitekwa siku ya Jumamosi walipokuwa wakisafiri kutoka mji mkuu Juba kwenda mji wa Pibor.

Hili ni tukio la tatu la aina hiyo ndani ya mwezi mmoja likiwa limepoteza maisha ya watu wengi tokea kuanza kwa mgogoro huo mwaka 2013.

Mkuu wa mashirika ya kibinaadam nchini Sudan Kusini Eugene Owusu ameelezea mauaji hayo kama uhalifu wa kutisha.

Wafanyakazi 12 wa mashirika ya kutoa misaada waneuawa mwaka huu, wakati huu ambapo wanajaribu kuelekea sehemu ambazo umaskini ni mkubwa kutokana na vita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *