Umoja wa Mataifa (UN) umekataa ombi la kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga kukagua matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti.

Msemaji wa umoja huo alikataa ombi hilo akisisitiza taarifa ya katibu mkuu wa Umoja huo Antonio Gutierrez ambapo amewataka viongozi wa Kenya kusuluhisha mgogoro wowote wa uchaguzi huo katika taasisi zinazofaa kikatiba.

Umoja huo umesema kuwa utatazama mpango mpya wa Raila Odinga ambao anapanga kutangaza siku ya Jumatano.

Wiki iliopita kiongozi huyo wa Nasa alitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kukagua matokeo hayo ya uchaguzi uliokamilika.

Kiongozi huyo wa upinzani alisema kuwa tume ya uchaguzi nchini IEBC ilikuwa chini ya shinikizo kali kutoka kwa maafisa wa serikali inayoongozwa na rais Kenyatta.

Kufuatia mauji ya mtaalam wa maswala ya kiteknolojia katika tume hiyo Chris Msando, wafanyikazi wengine waliogopa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *