Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanaolinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesema wamesaidia kuwasafirisha zaidi ya wapiganaji 100 kutoka Sudan Kusini hadi vituo vya afya nchini DRC kupokea matibabu.

Msemaji wa UN Stephane Dujarric amesema wapiganaji hao watiifu kwa kiongozi wa waasi Riek Machar walikuwa katika hali mbaya kiafya walipowasili nchini humo.

Machar mwenyewe alipewa usaidizi wa kimatibabu na wanajeshi wa UN baada ya kujeruhiwa mwezi uliopita katika mapigano nchini Sudan Kusini.

Jeshi linalomuunga kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar
Jeshi linalomuunga kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar

Baadaye aliondoka DRC na kuelekea Sudan na alitibiwa kwa muda na kuruhusiwa kuondoka hospitalini mwishoni mwa mwezi Agosti ingawa bado amesalia nchini Sudan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *