Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM) umemtaka mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Edward Lowassa kufuta mawazo kuwa Chadema itachukua madaraka.

Hayo yamesemwa na kaimu katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi taifa (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka.

Shaka amesema kuwa Lowassa anatakiwa kufuta fikra zake za Chadema kuishinda CCM hata kama UKAWA bado itakuwepo.

Alimtaka Lowassa kujua kuwa hata viongozi na wanachama wa upinzani hawamwafiki mwanasiasa huyo kwa asilimia kubwa kwani wapo viongozi aliowakuta ambao wametoa jasho jingi kuvijenga vyama vyao hivyo hawapo tayari kumpisha agombee tena urais.

Pia Kaimu katibu mkuu huyo amefafanua kuhusu kauri iliyotolewa na Lowassa kwa kusema kuwa Tanzania kuna ukandamizwaji wa demokrasia.

Kauli ya Shaka imekuja siku kadhaa baada ya Lowassa kuilalamikia Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam kuhairisha kongamano la Demokrasia lililotakiwa kufanyika katika ukumbi wa Anaotoglou jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *