Umoja wa Mataifa umedai kuwa umegundua makaburi 13 ya watu wengi kwenye jimbo la katikati ya nchi ya Congo la Kasai tangu mwanzoni mwa mwezi Machi.

Ugunduzi huo unafanya idadi ya makaburi ya aina hiyo yaliyogunduliwa kugikia 23.

Hata hivyo Umoja wa Mataifa umeshindwa kuyachunguza makaburi hayo na kubaini endapo yamechimbwa siku za karibuni au kama yana muda mrefu.

Inakadiriwa zaidi ya watu 400 wengi wao wanawake na watoto wameuawa kwenye mapigano baina ya jeshi la nchi hiyo na kundi la waasi.

Mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa wa Ofisi ya Muungano ya Haki za Binadamu ameliambia shirika la BBC, Jose Maria Aranaz, ametaka uchunguzi huru kufanyika ili kuwahakikishia wananchi pamoja na kuhakikisha watekelezaji wa mauaji hayo wanafikishwa mbele ya sheria.

Serikali ya Congo inapambana kuangusha upinzani wa kundi jipya la waasi la Kamwina Nsapu lililozuka baada ya Chifu wa eneo hilo kuuawa.

Pande zote zinashutumiwa kutenda uhalifu dhidi ya haki za binadamu ambapo mwezi uliopita wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa waliotumwa kuchunguza madai hayo walitekwa na kuuawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *