Wakazi wa jiji la Arusha na vitongoji vyake wamejitokeza kuaga miili ya wanafunzi 32 waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea siku ya Jumamosi.

Miili hiyo inaagwa leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo makamo wa Rais Samia Suluhu Hassan anaongoza waombolezaji kuwaaga wanafunzi hao.

Kutokana na umati mkubwa wa watu waliojitokeza katika uwanja huo, mageti yamefungwa kutokana na wingi wa watu kuongezeka uwanjani hapo.

a-town-2

Msiba huo umesimamiwa na Serikali ambapo itasafirisha kila mwili unapostahili kwenda kwa ajili ya maziko ya wanafunzi hao.

Wanafunzi hao wa shule ya msingi Lucky Vicent Academy ya jijini Arusha walipata ajali wakati wakielekea Karatu kwa ajili ya mitihani ya kujipima na shule ya Msingi Tumaini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *