Mshambuliaji wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu amesema kwamba anatarajia kurudi uwanja hivi karibuni kwenye Kombe la Shirikisho Afrika katika hatua ya nusu fainali baada ya kukosa mechi zote za mzunguko wa pili za Kundi A kutokana na kupona majeraha yake.

Ulimwengu hakucheza mechi za mzunguko wa pili Kundi A, dhidi ya Medeama nchini Ghana, MO Bejaia nchini Algeria na Yanga SC mjini Lubumbashi kutokana na kuwa majeruhi lakini sasa yuko fiti.

Kikosi cha TP Mazembe
Kikosi cha TP Mazembe

Baada ya kuongoza Kundi A, TP Mazembe itamenyana na Etoile du Sahel ya Tunisia wakati MO Bejaia itamenyana na FUS Rabat ya Morocco katika Nusu Fainali mechi za kwanza zikichezwa wikiendi ya Septemba 16 hadi 18, wakati marudiano yatakuwa wikiendi ya Septemba 23 na 25.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *