Ukaribu wa Alikiba na wapenzi wa Diamond

0
78

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba anaonekana kuwa karibu na wapenzi wa zamani wa mwanamuziki wenzakeDiamond Pltnumz.

Hamisa Mobetto na Tanasha Donna ambao tayari wamebwagana na Diamond, wana himaya yao katika ulimwengu wa Alikiba, huku warembo hao wanaupiga mwingi tu.

Hilo limezidi kujionyesha mara baada ya hivi karibuni Alikiba kuachia albamu yake ya tatu ‘Only One King’ yenye nyimbo 16. Je, ni lini na wapi na kwa namna gani Alikiba anapeta na hao Baby Mama wa Diamond kimuziki?

HAMISA MOBETO

Katika video ya wimbo wake ‘Dodo’ iliyotoka Aprili 2020, Alikiba ameupiga mwingi ndani yake kwa kuachia na Hamisa Mobetto ambaye ametokea kama video vixen licha ya kuachana na kazi hiyo kitambo ila Kiba akamrejesha tena.

Utakumbuka Septemba 2016 Hamisa aliipendezesha vilivyo video ya Diamond ‘Salome’ na kujizolewa umaarufu zaidi, baada ya hapo ndipo penzi lao la siri likachipuka hadi kupata mtoto mmoja.

TANASHA DONNA

Mara baada ya Dar es Salaam, Alikiba alienda pia kufanya listening party Nairobi, Kenya ambapo aliwaalika wasanii wa huko kama Otile Brown, Khaligraph Jones, Nyashinski Nameless, Wahu, na Tanasha.

Hata hivyo, siku kadhaa nyuma Alikiba alikuwa na Tanasha visiwani Zanzibar ambapo mrembo huyo aliungana na mwimbaji wa Kings Music, Tommy Flavour katika kushuti video ya wimbo wao ambao upo mbioni kutoka.

LEAVE A REPLY