Baada ya mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kuachiwa kwa dhamana kutokana na kukabiliwa na kesi ya kutumia dawa zakulevya, Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amempongeza mwenyekiti huyo.

Kupitia akaunti yake Instagram, Wema ameshindwa kuzizuia hisia zake baada ya kuweka picha ya Manji pamoja na kuandika maneno machache ya kumpongeza bada ya kupata dhamana hapo jana.

Manji ambaye ni mfanyabiashara maarufu nchini alipandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya ambapo aliachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10.

Wema alindika kama ifuatavyo huku akiambatanisha na picha ya mwenyekiti huyo. “Alhamdulillah… I said it once and I’ll say it again… What doesnt Kill you only makes you Stronger…. On behalf of Young africans niseme tu Asante Mungu kwa kututolea Manji wetu ndani.. Mule ndan sio sehemu nzuri kabisa jamani… Na anaekupeleka kule hawezi kua rafiki hata kidogo… Tena wa kukaa nae mbali kabisa… Inshallah all will be well… Nimefurahi kwakweli… Kama kawaida sitaki maoni… And naona hii ndo iwe mfumo mpya… Turn off comments basi… All in all, Welcome Back!”

Manji na Wema Sepetu ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kuelvya ambao walitakiwa kufika kituo cha polisi makao makuu (Central) makuu jijini Dar es Salaam.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *