Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Genk, Mbwana Samatta ameandika ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter unaosema siasa imekuwa cheap sana kwa viongozi wasasa.
Samatta ameandika hayo baada ya kituo cha TV cha Clouds Media kuvamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ijumaa iliyopita.
Kupitia akaunti yake hiyo Mbwana ameandika.“Ndiyo maana siasa imekuwa cheap maana viongozi wenyewe wana-hang out na akina Amber Lulu na Gigy Money” .