Ujumbe wa Diamond kwa Zari kufuatia kifo cha Ivan

0
1152

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amemtumia ujumbe wa kumfariji mpenzi wake, Zari kufutia msiba wa Ivan ambaye ni baba watoto watatu wa Zari The Bosy Lady.

Kumekuwa na mengi yanazungumzwa kwenye mitandaoni ya kijamii kuhusu Zari, Ivan na Diamond Platnumz na mengine yamepelekea kuwakera baadhi ya mashabiki wao wa damu.

Diamond ameandika ujumbe wa kumtia moyo Zari The Boss Lady na kuonyesha yupo naye pamoja katika kipindi hicho kigumu anachopitia.

Kupitia akaunti yake Instagram Diamond ameandika “Natamani ningekukumbatia badala ya kukutumia sms,najua upo kwenye wakati mgumu na ni mpweke, jua kwamba hauko mwenyewe, niko na wewe hapa usiku na mchana,”.

Ivan amefariki dunia Alhamisi nchini Afrika Kusini baada ya kuugua ugonjwa wa moyo kwa wiki kadhaa akiwa hospitali nchini humo.

LEAVE A REPLY