Aliyekuwa kocha wa Bayern Munich Carlo Ancelotti ameishukuru bodi ya timu hiyo kwa kumwamini pamoja na ushirikiano waliompa katika kipindi chote alichofundisha timu hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ancelotti ameandika “Imekuwa heshima kubwa kuwa sehemu ya historia ya Bayern Munich.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Napenda kuishukuru Klabu, Wachezaji na zaidi mashabiki wa kushangaza ambao sijawahi kukutana nao tangu nianze kufundisha soka”.

Mtalaam huyo wa ufundi mwenye miaka 58 alipoteza kibarua chake jana mchana baada ya bodi ya Bayern Munich kuketi na kocha huyo na kuazimia kutoendelea na mkataba wake uliokuwa unamalizika 2019.

Baadhi ya wachezaji wa Bayern Munich Thiago Alcantala, Frank Ribery, Robert Lewandowski na Arturo Vidal wamemshukuru Ancelotti kila mmoja akieleza kwa namna ambavyo amefaidika kuwa chini ya kocha huyo kwa msimu mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *